Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya jioni ya Jumapili mwezi (4 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (6 Februari 2022m) zimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Marjaa-Dini Shekhe Lutfullah Swafi Gulbaigani (q.s), aliyefariki siku ya Jumanne iliyopita.
Majlisi imefanywa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wanafunzi wa Dini na viongozi wa kijamii, bila kusahau viongozi wa Ataba mbili tukufu na watumishi wa Ataba hizo.
Marjaa Gulbaigani (q.s) alifariki siku ya Jumanne mwezi (28 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (1 Februari 2022m), watu wengi walijitokeza kushindikiza jeneza lake katika mji wa Najafu na Karbala, na amezikwa ndani ya jengo la malalo ya Imamu Hussein (a.s).
Kumbuka alikuwa mmoja wa Marajii-Dini wakubwa katika mji wa Qum, anavitabu vingi katika uwanja wa elimu.