Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuwa, kimeongeza maktaba (134) za (umma – binafsi – za sekula – za shule na za fani), pamoja na waandishi (466) wa kiiraq na vitabu vyao kutoka mkoa wa Najafu, kwenye orodha wa waandishi wa kiiraq.
Mkuu wa moja ya kituo cha maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Hassanain Mussawi amesema: “Kazi ya kuingiza taarifa za maktaba na waandishi inafanywa bila malipo, na inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa, inalenga kuandika taarifa nyingi zaidi, zitakazo mrahisishia msomaji kupata anacho hitaji sawa iwe ni maktaba au muandishi”.
Akaongeza kuwa: “Mradi wa faili la taarifa ni toghuti ya pekee hapa Iraq na katika nchi za kiarabu, na hutumika katika nchi nyingi duniani, aidha ni sehemu ambayo hukimbiliwa na watafiti”.
Wakati wa kuhitimisha ujumbe wake Mussawi akatoa wito kwa wasimamizi wote wa maktaba za serikali na binafsi pamoja na waandishi wanaopenda kuingizwa kwenye orodha hiyo wawasiliane na kituo.
Kumbuka kuwa faili la orodha ya waandishi wa kiiraq, linamilango mingi inayo elezea maktaba tofauti za Iraq, ndugu waandishi wanaweza kuwasiliana nasi kwa kupitia toghuti ifuatayo (http://afiqa.net) na zitaandikwa taarifa zao kwenye orodha bure.