Kuendelea kwa kazi ya kuvunja nyumba za Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kazi inayofanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuvunja baadhi ya majengo ya Jirani na Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kuongeza eneo bado inaendelea.

Nyumba zinazo vunjwa zipo upande wa mashariki mwa Ataba tukufu, upande wa uwanja wa -Alqami- na mlango wa Imamu Ali (a.s) -mlango wa kiganja cha mkono- hadi eneo la mlango wa Furaat.

Kazi inafanywa kwa umakini mkubwa, ukizingatia nyumba hizo vimeungana, na sehemu inayo zitenganisha na ukuta wa Atabatu Abbasiyya upo karibu, pamoja na kuwepo kwa nyumba zingine pembezoni mwake kwa upande wa nyuma.

Kazi yote inafanywa na kamati ya mafundi, na imeweka utaratibu mzuri wa ubomoaji, wanafanya kazi kwa umakini na tahadhari kubwa na wanatumia vifaa Madhubuti, wanahakikisha hawaathiri majengo mengine.

Kumbuka kuwa kazi ya mradi huu inatokana na kuwepo kwa msongamano mkubwa wa mazuwaru, hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, eneo hilo hujaa watu hadi huathiri utekelezaji wa ziara na ibada na wengine hushindwa kuingia ndani ya Ataba tukufu kutokana na ukubwa wa msongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: