Kufanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa awamu ya kwanza wa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Nafaru chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa awamu ya kwanza wanaoshiriki kwenye mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya sita, katika semina hizo wamefundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani na kanuni za tajwidi.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mitihani wamefanyiwa katika shule ya Ayatullahi Sayyid Muhsin Hakiim (q.s), ilikua ya aina mbili (nadhariyya na vitendo), wanafunzi wa hauza kutoka ngazi tofauti wameshiriki, mtihani huu unafanywa baada ya kumaliza semina za Qur’ani hatua ya kwanza, kwa lengo la kupima kiwango cha washiriki na uwelewa wao”.

Akaongeza kuwa: “Hatua hii itafuatiwa na hatua zingine zitakazokua na mada tofauti, kama vile maarifa ya Qur’ani, tafiti katika Qur’ani, chini ya walimu waliobobea katika mada hizo”.

Akasisitiza kuwa: “Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, awamu hiyo itakamilisha awamu zilizo tangulia, tayali tumesha andaa ratiba kamili ya semina hizo, na wakufunzi wenye uwezo wa kuwasilisha mada kwa njia rahisi, na kumuwezesha mwanafunzi wa Dini anayeshiriki kwenye semina hizi kuwa na uwelewa mkubwa wa mambo yanayo husiana na Qur’ani”.

Kumbuka kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini, ni mradi muhimu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, mradi huu unanafasi kubwa ya kurekebisha jamii katika sekta ya Tablighi, sambamba na kufanyia kazi maelekezo ya Mtume (s.a.w.w) kwa umma wake, pale aliposema nawaachieni vizito viwili Qur’ani tukufu na kizazi kitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: