Balozi wa cheki nchini Iraq Mheshimiwa Bito Shatibanki na wajumbe aliofuata nao leo siku ya Jumanne, wametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini pamoja na viongozi wengine.
Wameongea mambo mengi yanayo husu Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi na utoaji wa huduma kwa mazuwaru wanaotembelea mji mtukufu wa Karbala, sambamba na harakati mbalimbali zinazo simamiwa na kufadhiliwa na Ataba tukufu.
Kisha balozi akatembelea makumbusho ya Alkafeel akiwa Pamoja na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, na rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Huquqi Muhammad Ali Azharu hadi katika jingo la Al-Ameed na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Mheshimiwa balozi wa Cheki na wajumbe aliokua nao. Wamesikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa miradi hiyo, walio eleza huduma wanazo toa na mitambo waliyo nayo.
Mwisho wa ziara yake Waziri wa Cheki ameuthibitishia mtandao wa Alkafeel, furaha yake kwa kupata nafasi ya kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha amesifu na kupongeza miradi aliyo tembelea, amesema kuwa ni miradi muhimu na inayotekelezwa kisasa, hususan hospitali ya rufaa Alkafeel.