Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaendesha mradi wa kukuza uwezo kwa mara ya kwanza katika vitongaji na mitaa

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu (inaendesha mradi wa kujenga uwezo katika vitongoji na mitaa).

Sayyid Muhandi Almayali mkuu wa Maahadi amesema: “Chini ya bendera ya mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s), umeanza utekelezaji wa (mradi wa kujenga uwezo kwa mara ya kwanza katika vitongoji na mitaa), tumeanza na (mtaa wa Radhawiyya)”.

Akaongeza kuwa: “Washiriki wamechaguliwa kwa kuzingatia muongozo wa Maahadi na muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika mtaa huo, katika mradi huu watafundishwa (kanuni za tajwidi, mbinu za ufundishaji, naghma za Qur’ani pamoja na mafundisho ya kiroho kutoka katika Qur’ani tukufu), ndani ya kipindi cha miezi miwili”.

Akafafanua kuwa: “Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa (Mwanafunzi ananishauri kuongeza harakati za Qur’ani katika vitongoji na mitaa)”.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendelea kufanya semina mbalimbali kupitia matawi yake, pamoja na harakati zingine zinazo lenga kukuza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: