Blog ya Alkafeel ni miradi wa kitamaduni unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Blog ya Alkafeel ni miongoni mwa madirisha ya hauza ya kimtandao ya Maahadi ya Turathi za Mitume (a.s), chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huo unafanya kazi ya kukusanya kazi za waandishi kwa kutumia jukwaa la mitandao.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa wahariri Shekhe Hussein Asadi, amesema: “Mrari huu ulianza mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka (2018) kwa jina la (kalamu za maarifa), kisha baadae jina likabadilishwa na kuwa (Blog ya Alkafeel), kwa lengo la kuandika tafiti na makala katika sekta mbalimbali za maisha, kama vile: (jamii, itikadi, tamaduni na zinginezo), lengo kuu ni kukusanya kazi zote zinazofanywa na kalamu kwenye karatasi ya (waandishi wa mnyweshaji wenye kiu Karbala)”.

Akaongeza kuwa: “Blog ya Alkafeel ni mradi unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kuhifadhi utambulisho wa elimu na utamaduni, usiharibiwe kwa kuingiliwa na tamaduni za kigeni katika jamii, aidha mradi huu unalenga kuhuisha kazi ya kalamu na kubainisha thamani yake katika mtazamo wa kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani na sunna, sambamba na kuangalia msimamo usiokua wa kiislamu, kwa kuangalia uzowefu wa magharibi katika swala hilo, japokua tunatofautiana katika madhumuni”.

Akafafanua kuwa: “Milango ya Blog ikowazi kwa ajili ya kupokea Makala zote za watafiti zinazo lenga kufikia lengo lake, ikiwa ni pamoja na Makala za mambo ya kifamilia, visa, mitazamo, matukio ya kidini, mambo ya kijamii, kiitikadi, Makala zilizo tafsiriwa, visa vya Watoto, malezi, utafiti kuhusu Imamu Mahadi (a.f), nukta za kielimu katika Qur’ani, mambo mashuhuri ya kijamii, mwanamke baina ya uislamu na umagharibi, ubainifu na ufasaha katika maneno ya Ahlulbait (a.s)”.

Akaendelea kusema kuwa: “Kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu, tumeanza kuandika kwa lugha ya kiingereza, kwa lengo la kufikisha fikra za Ahlulbait (a.s) kwa wageni wasiofahamu lugha ya kiarabu, na kwa wanaotafuta ukweli”.

Kuangalia Blog au kuwasiliana na wahudumu wake tumia link zifuatazo:

Toghuti ya Blog tumia link hii:

https://alkafeelblog.edu.turathalanbiaa.com/

mtandao wa telegram:

✅ https://t.me/turathalanbiaa_alkafeelblog

Ukurasa wa facebook:

✅ facebook.com/alkafeelblog

Mtandao wa Instagram:

✅ https://www.instagram.com/alkafeelblog/

Blog ya Alkafeel:

✅ https://play.google.com/store/apps/details?id=com.turath.blog

Unaweza kuangalia mtandao wa kiengereza kwa kutumia link ifuatayo:

https://t.me/AlKafeelBlog
Na unaweza kuwasiliana na uongozi kwa kutumia anuani ifuatayo:

@Alkafeelbloghusbot
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: