Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaendelea na mradi wa semina za Qur’ani kwenye vyuo vikuu na Maahadi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha mradi wa Qur’ani kwenye vyuo vikuu na Maahadi.

Semina ya safari hii inawashiriki zaidi ya (70) kutoka chuo kikuu cha Kufa/ kitivo cha malezi mchanganyiko na malezi ya msingi.

Semina imehusisha masomo ya tajwidi mara tatu kwa wiki, chini ya ukufunzi wa Ustadh Hussein Saidi Alhabubi.

Tambua kuwa mradi unashughuli nyingi, miongoni mwa shughuli zake ni: (mashindano, nadwa, hafla, semina za Qur’ani, maonyesho ya picha, safari za kidini -kwenda katika Ataba za Karbala-).

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake yote, ni sehemu muhimu ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha masomo ya Qur’ani na kusaidia kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: