Mafunzi selemala wanaofanya kazi katika kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukifu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kutengeneza mapambo ya mbao ya sehemu za vyumba vya madirisha katika dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) kwa ndani, baada ya kumaliza kutengeneza paa la ndani.
Rais wa kitengo hicho Sayyid Nadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya mbao kwenye dirisha hilo imefika hatua nzuri, kazi hii inaenda sambamba na kazi zingine za sehemu za madini, asilimia kubwa ya kazi zipo mwishoni, vipande vya vyumba vya dirisha vimefika (14) kuzunguka dirisha pande zote, tumeanza kazi ya kutengeneza mapambo ya mimea yenye randi nzuri inayo endana na mapambo yaa paa, na kufanya dirisha lote kuwa na muonekano mmoja”.
Akaongeza kuwa: “Kazi ya kuweka mapambo inafanywa kwa umakini mkubwa, kila kipande cha dirisha kinawekwa pambo la vyumba vya madirisha lenyo umbo la upinde, lenye urefu wa (sm 143), sehemu kubwa zaidi na upana wa (sm 80), sehemu yenye upana zaidi, sehemu ya juu inazungukwa na ufito wa pambo wenye maandishi, unaoshikiliwa na nguzo kuu za chini”.
Akafafanua kuwa: “Nakshi na mapambo ya mbao yametengenezwa kwa umaridadi mkubwa, kazi hiyo imefanywa na mafundi mahiri tena kwa weledi mkubwa kutokana na utukufu wa mwenye malalo takatifu, na kufanya sehemu hizo ziendane na sehemu zilizotiwa madini”.
Akamaliza kwa kusema: “Katika utengenezaji wa mapambo hayo hazikutumika rangi za kawaida, bali imetumika rangi ya mbao halisi zilizo agizwa kutoka sehemu tofauti duniani zenye ubora wa hali ya juu, aina mbalimbali ya mbao zimetumika katika kazi hiyo tukufu”.
Kumbuka kuwa utengenezaji wa vyumba vya madirisha unapita katika hatua mbalimbali, kuanzia utengenezaji wa vipande hivyo hadi kwenye kuviunganisha katika umbo la dirisha pamoja na sehemu za madini ya fedha, na mwisho vinafungwa kwenye umbo kuu la dirisha, kazi zote zinafanywa kwa umakini mkubwa, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa katika muundo huu.