Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imeandaa shindano kuhusu Imamu Ali (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa shindano la wanawake kuhusu Imamu Ali (a.s), kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kunako sadifu mwezi kumi na tatu Rajabu-Aswabu chini ya kauli mbiu isemayo (Ali Imamu wa mapenzi na kusamehe).

Maahadi imesema kuwa masharti ya shindano ni:

  • Shindano ni maalum kwa wanawake peke yao.
  • Ujumbe usiwe umetolewa kwenye intanet au kitabu.
  • Ujumbe usizidi maneno (200).
  • Ujumbe usiwe na makosa ya kilugha na kiuandishi.
  • Mshiriki aandike jina lake halisi.
  • Ujumbe aundikwe kwa program ya word na utumwe kwenye telegram kwa nama ya simu (07832464904).
  • Siku ya mwisho ya kupokea jumbe za washiriki ni Jumapili, (11 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (13 Februari 2022m).
  • Ujumbe ambao hautakamilisha masharti tajwa hauzingatiwa.

Matokeo yatatangazwa siku ya kuadhimisha mazazi matakatifu, baada ya jumbe zote kuwasilishwa mbele ya kamati ya majaji na kuchujwa, kisha watachaguliwa washindi watatu watakao pewa zawadi na kuandikwa jumbe zao kwenye machapisho maalum ya Maahadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: