Mwezi kumi Rajabu ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi kumi Rajabu-Aswabu ni siku aliyozaliwa Imamu wa tisa miongoni mwa Maimamu watakatifu, naye ni Muhammad Aljawaad (a.s) mwaka 195h.

Imamu Aljawaad jina lake kamili ni Muhammad mtoto wa Ali mtoto wa Mussa mtoto wa Jafari mtoto wa Muhammad mtoto wa Ali mtoto wa Hussein mtoto wa Ali mtoto wa Abu Twalib (a.s), mama yake ni bibi Sakina Marsiyya na inasemekana ni Khaizarani, na mke wake alikua ni bibi Sumana kutoka Moroko, alikua kituo cha ukarimu kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao.

Imepokewa katika kitabu cha (Manaqibu Aalu-Abu Twalib) cha Ibun Shahri Aashuub kuwa: Mama yake Abu Jafari (a.s) alipokaribia kujifungua, Imamu Ridhwa (a.s) alimwita dada yake, akasema: (Ewe Hakimah hudhuria Mazizi yake) akamuingiza ndani (a.s), akawasha taa na kufunga mlango.

Baada ya muda akajifungua, Imamu Ridhwa (a.s) akafungua mlango, akamchukua mtoto na kumuweka miguuni, akasema: (Ewe Hakima mfunike), alipofika siku ya tatu, aliangalia juu, halafu akaangalia upande wa kulia na kushoto, akasema (a.s): (Nashuhudia kuwa hakuna Mungu ispokua Allah na hakika Muhammad ni mtume wa Allah).

Nikaenda kwa Abul-Hassan (a.s) nikamuambia: (Nimesikia maneno ya ajabu kwa huyu mtoto) akauliza (umesikia nini)? Nikamuambia nilicho sikia. Akasema (a.s): (Ewe Hakima, utaona ajabu nyingi).

Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) alizaliwa mwezi kumi Rajabu mwaka wa 195h, akapewa jina la (Muhammad) na jina la kuniya la (Abu Jafari).

Kuzaliwa kwake (a.s) kulileta shangwe na furaha katika jamii ya wafuasi wao, kulituliza roho zao na kuondoa shaka iliyokua imeanza kuingia kwa baadhi yao.

Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) amekulia katika nyumba ya Utume na Uimamu, nyumba tukufu ambayo Mwenyezi Mungu amewatunuku waislamu, amelelewa katika nyumba hiyo na kujifunza tabia njema kutoka kwa baba yake Imamu Ridhwa (a.s), naye alisimamia yeye mwenyewe malezi ya mtoto wake mtukufu, alikua pamoja nae kila mahala, hadi akawa mkubwa (a.s), akiwa amesoma elimu nyingi kutoka kwa baba yake (a.s), iliyo muwezesha kufundisha wanachuoni na wanafunzi njia za usomaji wa sheria za Dini tukufu ya kiislamu, akahimiza wanafunzi wake waandike mambo yote aliyo wafundisha na waliyosoma kwa wazazi wake watukufu.

Miongoni mwa majina yake ya sifa (a.s) anaitwa (Aljawaad, Ataqiyyu, Alqaanii, Almurtadhwa, Almuntajabu) na mashuhuri zaidi ni (Aljawaad), kutokana na wingi wa kutoa kwake, pia alikua anaitwa Mlango wa kukubaliwa haja (Baabu Muraad), kutokana na watu wengu kukubaliwa haja zao mbele ya kaburi lake takatifu, alikufa (a.s) akiwa na umri wa miaka (25), uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: