Idara ya Qur’ani imefanya tukio la kitamaduni kwa wanawake katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Aljawadi (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya wanawake, imefanya tukio la kitamaduni katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Aljawadi (a.s).

Kiongozi wa idara ya Qur’ani bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel harakati zinazo fanywa na idara hiyo kila wiki, katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) -sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim a.s- na kuhudhuriwa na mazuwaru na wanawake wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya wiki hii ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mihadhara miwili yenye mada za kimalezi na kijamii, mada ya kwanza ilijikita katika mambo ya kifiqhi na kutoa shuhuda kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), na mhadhara wa pili ulijikita katika malezi, ambapo imeelezewa Hadhithi-Kisaa na jinsi ya kunufaika nayo katika Maisha ya kila siku, kwa njia za kisasa sambamba na mahitaji ya kila kundi katika Maisha”.

Akaendelea kusema: “Ratiba hiyo pia ilikua na maswali pamoja na shindano kuhusu Imamu Aljawadi (a.s), shughuli hiyo ilipambwa na mashairi na tenzi”.

Akafafanua kuwa: “Watoto walikua na nafasi maalum katika ratiba hiyo, mwisho kabisa watu wote waliinua mikono na kusoma dua Faraji ya imamu wa zama (a.f)”.

Shughuli hiyo imepata muitikio mkubwa, washiriki wameshukuru kupata nafasi hiyo tukufu ya kushiriki kwenye tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: