Katibu mkuu wa Atabatu Askariyya ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kumpongeza katibu mkuu wake

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Askariyya ukiongozwa na katibu mkuu Dokta Muhammad Qassim na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, wametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya leo siku ya Jumamosi (10 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (12 Februali 2022m), ugeni huo umepokewa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya yukufu Mhandisi Abbasi Mussawi na wajumbe wa kamati yake.

Ugeni huo baada ya kumaliza kufanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya malalo takatifu wakiwa pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, wakaelekea katika ukumbi wa utawala kwenda kutoa pongezi zao kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kumtakia mafanikio mema katika kazi yake takatifu.

Naye Sayyid Mustwafa katika kikao hicho ameomba kuimarisha ushirikiano baina ya Ataba mbili takatifu, aidha ameshukuru wageni wake kuja kufanya ziara na kumpongeza kwa kupewa madaraka hayo, akaomba mafanikio mema ya kuzitumikia Ataba takatifu na mazuwari wake.

Mwisho wa kikao wageni wakakabidhi zawadi, ambayo ni bendera kutoka kwenye malalo ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s) kwa Mheshimiwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na vitu vingine vya kutabaruku na malalo hiyo takatifu, kisha wageni wakaaga na kuombewa kukubaliwa ziara yao na kuwatakia kurudi salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: