Kamati imesema kuwa baada ya kupokea majibu yamefanyiwa uchambuzi na kupatikana majibu sahihi ambayo yatapigiwa kura saa moja jioni siku ya Jumatatu (12 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (14 Februari 2022m), katika hafla kubwa itakayofanywa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Sharti la kupokea zawadi mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla hiyo, na awe na kitambulisho chenye jina na picha yake, asipokuwepo au akakosa kitambulisho atachaguliwa mshindi mwingine kwa njia ya kura.
Tambua kuwa zawadi iliyo andaliwa ni:
- - Hela dinari laki mbili na elfu hamsini (250,000).
- - Kifurushi cha zawadi za kutabaruku na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Idadi ya washiriki hadi wakati tunafunga kupokea majibu siku ya Jumamosi ilikua ni (2,935), wametolewa washiriki (29) ambao hawakukamilisha masharti, na kupata majibu sahihi yaliyo kamilisha masharti yote (531).
Majina ya waliojibu sahihi yapo kwenye picha ya Habari.