Maandalizi ya kupandishwa bendera katika usiku wa kuzaliwa kwa Alawiyya (Ali bendera ya uongofu) yawasili katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Imewasili katika Atabatu Abbasiyya tukufu bendera iliyotolewa na Atabatu Alawiyya ambayo imeandikwa (Ali bendera ya uongofu) kama sehemu ya maandalizi ya kuipandisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) jioni ya kesho siku ya Jumatatu (12 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (14 Februari 2022m).

Bendera hiyo imepokelewa na rais wa kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Muhammad Ali Azhar kutoka kwa ugeni maalum uliokuja kutoka Atabatu Alawiyya tukufu, ukiongozwa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Salim Jaswani.

Dokta Jaswani amesema: “Ujio wetu umetokana na maelekezo ya katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Issa Khurasani, kuja kukabidhi bendera ya kiongozi wa waumini (a.s) aliyo andikwa (Ali bendera ya uongofu), kama maandalizi ya kupandishwa kwake katika maeneo matakatifu (kwenye kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na kwa Maimamu wawili Alkadhimaini na Askariyaini -a.s-), katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini (a.s) mwezi kumi na tatu Rajabu-Aswabu”.

Akaongeza kuwa: “Kukabidhi bendera hii kwa Ataba tofauti ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya mzaliwa wa Alkaaba, ambapo kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe aliyo zaliwa (a.s)”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa kufanya mambo tofauti, ikiwa ni pamoja na hafla kubwa itakayo fanywa tarehe ya siku aliyo zaliwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu pamoja na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: