Atabatu Abbasiyya tukufu inatarajia kufanya hafla ya kuwapa zawadi mayatima katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa baba yao

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inatarajia kufanya hafla siku ya Jumanne (13 Rajabu 1443h) kwa ajili ya kuwapa zawadi mayatima (150) kutoka taasisi mbalimbali zinazo lea mayatima katika mkoa wa Karbala, kufuatia maadhimsho ya kumbukumbu ya kuzaliwa baba wa mayatima kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhusein Alyaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hafla hiyo itafanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha mahusiano, kitengo cha utumishi, kitengo cha Habari na utamaduni na kitengo cha Habari”.

Akafafanua kuwa: “Hafla inalenga kutia furaha katika nafsi za mayatima hao, na kuonyesha nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika kushirikiana na taasisi za kiraia, zikiwemo taasisi zinazolea mayatima”.

Akaongeza kuwa: “Hafla hii ni sehemu ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kuadhimisha na kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s), aliyekua analea mayatima anakesha kwa kuhakikisha wanapata raha, hakika alikua baba mpenzi kwao”.

Akamaliza kwa kusema: “Tumeandaa kamati maalum inayosimamia hafla hiyo, ikiwa ni pamoja na kusimamia zawadi watakazo pewa kutoka kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: