Chuo kikuu Al-Ameed kinafanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini (a.s) kwa kuhudhuriwa na kundi la watoto mayatima

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya kuadhimiza mazazi ya kiongozi wa waumini Ali (a.s), na kuhudhuriwa na kundi la watoto yatima kutoka taasisi ya (Kidogo ni bora kuliko kukosa) pamoja na wakufunzi wa chuo na wanafunzi wao.

Hafla hiyo imesimamiwa na kitengo cha maelekezo ya kinafsi na muongozo wa kimalezi katika chuo hicho, chini ya usimamizi wa rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s) katika chuo hicho, asubuhi ya Jumapili (11 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (13 Februari 2022m).

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo, baada yake makamo rais wa chuo Dokta Alaa Jibri Mussawi akazungumza kuhusu mazazi ya Ali bun Abu Twalib (a.s), na msaada wake kwa wanaadamu pamoja na jinsi alivyo pambana katika kufundisha Dini tukufu, akataja baadhi ya sifa zake (a.s) ikiwa ni pamoja na mapenzi makubwa aliyokua nayo kwa mayatima.

Kisha bwana Azhar Rikabi kiongozi wa taasisi ya (kidogo ni bora kuliko kukosa) akaongea, sambamba na kutambulisha harakati zinazo fanywa na taasisi yake katika kulea mayatima, akatoa shukrani nyingi kwa chuo kikuu cha Al-Ameed na kwa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mualiko huu na hafla hii tukufu.

Hafla imepambwa na mashairi pamoja na michezo mbalimbali ya Watoto yatima, hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi mbalimbali kwa mayatima, kisha wakatembea kuangalia mazingira ya chuo kikuu cha Al-Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: