Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s), jioni ya Jumatatu (12 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (14 Februari 2022m).

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ammaar Hilliy, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa kusimama kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukawasilishwa ujumbe kutoka uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa niaba na Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Hafla imepambwa na kaswida na mashairi kutoka kwa Hamza Hussein Abadi na Mustwafa Rikabi, halafu yakasomwa mashairi ya Sha’abi na mshairi Mustwafa Rikabi na Farasi Asadi na Abu Muhammad Almayahi.

Mwisho zikapigwa kura za washiriki wa shindano la (mzaliwa wa Alkaaba -a.s), lililo andaliwa na kitengo cha habari kwa kushirikiana na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tambua kuwa vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu vimeshirikiana kufanya hafla hii, chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini, na ushiriki wa kiongozi mkuu wa kisheria kupitia muambata wake Dokta Afdhalu Shami.

Miongoni mwa vitengo vilivyo shiriki ni: kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi, kitengo cha uhusiano, kitengo cha Habari, kitengo cha usimamizi wa haram tukufu, kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kitengo cha Habari na utamaduni, kitengo cha utunzaji wa haram tukufu, kituo cha matangazo na masoko Alkafeel, kitengo cha utumishi, kitengo cha Dini na vitengo vingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: