Kufanya shindano la (Fustwaatul-Qur’ani) kwa wanawake

Maoni katika picha
Idara ya masomo ya Qur’ani chini ya ofisi ya shule za Alkafeel za Dini upande wa wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya shindano la (Fustwaatul-Qur’ani) la kuhifadhi surat Baqarah, kwa wanafunzi walioshiriki katika semina za siku za nyuma.

Jumla ya wanafunzi (26) wameshiriki kwenye shindano hilo, baada ya kuhitimu kwao semina za kuhifadhi sura hiyo tukufu na kuwa na utayari wa kushiriki shindano hili, lililofanywa chini ya usimamizi wa kitengo cha Qur’ani, wamesikilizwa ubora wa hifdhu, naghma, sauti, hukumu, kuanza na kusimama.

Maswali yameulizwa kwa kufuata masharti ya shindano, sharti kubwa ni kwamba mshiriki lazima awe amehifadhi vizuri surat Baqarah, kwa mujibu wa kamati, matokeo yalikua mazuri sana, wanafunzi wamehifadhi na kusoma kwa usahihi.

Washindi watapewa zawadi kwenye hafla itakayo fanywa na idara ya shule za Alkafeel za Dini upande wa wanawake, katika kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Kumbuka kuwa idara ya masomo ya Qur’ani hufanya semina mara nyingi za Qur’ani kwa wasichana wenye umri tofauti, miongoni mwa semina hizo zinahusu kuhifadhi, hukumu za usomaji, tajwidi na mengineyo, hivi karibuni imefanya semina ya kuhifadhi surat Baqarah, kwani kudumu katika kusoma sura hiyo kuna fadhila nyingi, na baadhi ya aya za sura hiyo zina umaalum mkubwa, sambamba na kuwawezesha wanasema wetu kwenda kushiriki kwenye mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa, aidha wataendelea kuhifadhi sura zingine ndani ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: