Katika kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya mwezi (13 Rajabu-Aswabu 1443h), sawa na tarehe (15 Februari 2022m), imefanya majlisi chini ya anuani isemayo: (kwa uongofu wao fuateni), katika maadhimisho hayo wameshiriki kundi kubwa la mazuwaru watukufu.
Maadhimisho yamehusisha usomaji wa hadithi zinazo taja sifa ya mbora wa mawasii (a.s) na baadhi ya nasaha na maelekezo ya kifiqhi na kiaqida yaliyo andaliwa kwa ajili ya tukio hili tukufu.
Aidha washiriki wamepewa vipeperushi vyenye maswali kwa ajili ya kuyajibu, na washindi wamepewa baadhi ya zawadi za kutabaruku kutoka ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kusoma Qur’ani tukufu kwa ajili ya muadhimishwa mtukufu (roho zetu ziko tayali kujitolea kwa ajili yake).
Shughuli hiyo imepata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki, wamepongeza na kushukuri kwa kupewa nafasi ya kushiriki kwenye tukio hili adhim.
Kumbuka kuwa tukio hili ni moja ya shughuli za kidini zinazopewa umuhimu mkubwa na idara ya Qur’ani, kwa ajili ya kufaidika na matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kuingiza furaha katika nyoyo za waumini, aidha ni sehemu ya kufanyia kazi kauli isemayo (wafuasi wetu hufurahi kwa furaha zetu).