Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umewasili katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), kwa ajili ya kufanya baadhi ya kazi katika Ataba hiyo takatifu, baada ya kukanyaga ardhi ya mji mbuu wa Sirya Damaskas mikono yao ikashika chupa za mauwa, kwa ajili ya kutoa pongezi kwa mwenye malalo takatifu na mazuwaru wake kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa baba yake kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Kiongozi wa ugeni na rais wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Haji Khaliil Hanuni ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), umeundwa ujumbe wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka vitengo tofauti, kuja kufanya baadhi ya shughuli katika malalo ya bibi Zainabu (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Wakati wa kuwasili kwetu kwenye malalo yake tumeshika chupa za mauwa kwa ajili ya kupamba malalo takatifu ya bibi Zainabu (a.s) sambamba na kutoa pongezi kupitia utoaji wa mauwa kutoka kwa msimamizi wake Abulfadhil Abbasi (a.s), idadi kubwa ya mauwa imegawiwa kwa mazuwaru kwa ajili ya kuingiza furaha katika nyoyo zao”.
Akamaliza kwa kusema: “Ugeni utafanya shughuli mbalimbali na mwazo wake ndio huu utoaji wa mauwa, tutaendelea kutoa huduma hizo hadi siku ya kumbukumbu ya kifo chake ambayo ni tarehe kumi na tano ya mwezi huu”
Kumbuka kuwa hii sio mara ya kwanza kushiriki Atabatu Abbasiyya katika kutoa huduma kwenye malalo hii, imekua ikishiriki mara nyingi katika kila mwaka.