Kufanya shindano la mnara wa uongofu kwa wanawake

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya shindano la wanawake kwa anuani isemayo: (Mnara wa uongofu), kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) sambamba na kuangazia historia ya muadhimishwa (a.s).

Ushiriki unafanywa kupitia link ifuatayo:

https://forms.gle/zhFi6DgabGVAz2sf6

itaundwa kamati itakayo simamia upokeaji wa majibu na kuchambua majibu sahihi, kisha watachaguliwa washindi watatu kupitia upigaji wa kura mubashara, katika hafla itakayo fanywa ndani ya ukumbi wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Karbala.

Sharti la kuchukua zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla hiyo wakati kura zinapogigwa na wakati wa kutangaza matokeo ya kura, aje na kitambulisho chenye majina yake na picha yake, asipo kamilisha masharti hayo atachaguliwa mshindi mwingine kwa njia hiyohiyo ya kura.

Kumbuka kuwa shindano hili ni moja ya mashindano mengi yanayo ratibiwa na kituo, katika kumbukumbu za kuzaliwa au kufariki kwa Imamu, ili kuongeza uwanja wa kuwajua na kupanua wigo wa utafiti kuhusu watu hao waliokirimiwa na Mwenyezi Mungu na akawafanya kuwa watu bora baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: