Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chuni ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), kwenye ofisi zake na kuhudhuriwa na wanafunzi wengi wa Maahadi na wageni waalikwa kutoka nje.
Hafla ilikua na mambo mengi, ilifunguliwa kwa usomaji wa Qur’ani ambao walishiriki wanafunzi wa Maahadi Alyaafiyaat, yakafuata maswali kuhusu Qur’ani ambayo washiriki walitakiwa kujibu.
Hali kadhalika kulikuwa na kipengele cha kaswida na tenzi kuhusu kiongozi wa waumini (a.s) chini ya usimamizi wa kikosi cha Nab’ul-Juud, shangwe na furaha ilitanda kwa watu wote waliohudhuria, hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la (Alqur’anu-Naatwiqu) lililosimamiwa na Maahadi siku chache zilizo pita.
Vituo vya tawi la Maahadi katika mkoa wa Baabil ambavyo ni: (kutuo cha Aufi, kituo cha Maradu-Shamsi na kituo cha Wilaya ya Qassim), vimefanya hafla zilizohusisha vipengene tofauti, kama vile mawaidha, kaswida na mashairi yaliyo weka mazingira ya furaha katika maadhimisho haya matukufu.