Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya.. umefanywa ugawaji wa viti-mwendo vya kisasa kwa majeruhi wa jeshi la serikali

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imegawa viti-mwendo vya kisasa kwa majeruhi wa jeshi la serikali, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, huu ni muendelezo wa misaada tofauti iliyotolewa miaka ya nyuma kwa kundi hili la wahanga.

Kiongozi wa hospitali Sayyid Muhammad Haadi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika mheshimiwa Sayyid Swafi anatilia umuhimu mkubwa swala la kusaidia familia za mashahidi na majeruhi wa wanajeshi wa serikali na Hashdu-Sha’abi, tangu ilipotolewa fatwa ya jihadi ya kujilinda hadi sasa, chini ya maelekezo yake hospitali imekua ikitoa huduma za matibabu bure kwao tangu mwaka 2015m hadi sasa”.

Akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu itaendelea kuwa ngome Madhubuti kwa wahanga hawa waliojitolea kwa ajili ya taifa hili, hakika tunacho toa kwao ni kidogo kushinda wanavyo stahiki, tutaendelea kusaidia kadri ya uwezo wetu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.

Naye mkuu wa kitengo cha upasuaji na kiongozi wa ufuatiliaji wa maswala ya mashahidi na majeruhi katika wizara ya mambo ya ndani luteni Hakim Wais amesema kuwa: “majeruhi alijitolea kitu muhimu zaidi kwake kwa ajili ya taifa, misaada wanayopewa na Atabatu Abbasiyya sio mipya, bali ni muendelezo wa utoaji wa misaada”.

Majeruhi wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na wahudumu wake pamoja na uongozi wa hospitali ya rufaa Alkafeel, wakasema kuwa wamekuwa wakisaidiwa na Ataba tukufu tangu walipoanza kupigana vita dhidi ya magaidi hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: