Mwezi kumi na tano Rajabu-Aswabu ni kumbukumbu ya kifo cha mfanya ibada mkubwa wa Aalu-Ali (a.s), Aqilatu-Twalibina bibi Zainabu Kubra (a.s), aliye kulia katika nyumba ya elimu na maarifa na mashukio ya wahyi, aliishi baina ya shule ya Utume na Uimamu na akahitimu katika shule hizo mbili takatifu.
Amelelewa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wasii wake Ali bun Abu Twalib (a.s) na mama wa baba yake Fatuma Zaharaa (a.s) mbora wa wanawake wa duniani na Hassan na Hussein (a.s) mabwana wa vijana wa peponi, mwenye kuhitimu katika shule hiyo anafaa kuwa kiigizo chema kwa mwanamke mwema wa kiislamu.
Bibi Zainabu (a.s) alikua sawa na mama yake Swidiqah Zaharaa (a.s) katika kufanya ibada, alikua anafunga, anaswali na kusoma dua kwa wingi, muda mwingi wa usiku aliswali tahajudi na kusoma Qur’ani tukufu, hakuacha kufanya hivyo hata katika siku ngumu kwake kama siku ya mwezi kumi na moja Muharam, kutoka kwa Fadhil Naini Burjudi anasema: Hussein (a.s) alipomuaga dada yake kwa mara ya mwisho alisema: “Ewe dada yangu usinisahau katika sunna za usiku”.
Hali kadhalika alikua ni mfano mkubwa katika kujihifadhi, Yahya Almazini anasema: Nilikua Jirani na kiongozi wa waislamu (a.s) katika mji wa Madina tena karibu na nyumba aliyokua anakaa binti yake Zainabu, sikuwahi kumuona wana kusikia sauti yake, alikua anapotaka kwenda kutembelea kaburi la babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), anatoka usiku huku Hassan akiwa kuliani kwake na Hussein Kushotoni kwake na kiongozi wa waumini mbele yake, wakikaribia kaburi tukufu anatangulia kiongozi wa waumini (a.s), kisha anapunguza mwanga wa taa, Hassan akamuuliza kwa nini anafanya hivyo, akasema: Naogopa watu wasimuangalie dada yako Zainabu, Imamu Hassan alikua akitembelewa na Zainabu anasimama kwa kumheshimu, na anamkaribisha kwenye kiti chake.
Bibi Zainabu (a.s) alishuhudia mauaji wa Karbala, ambapo waliuawa Watoto wake na ndugu zake mbele ya macho yake, lakini aliendelea kufanya Subira mbele ya Mwenyezi Mungu, Subira yake inaonekana wazi kwa namna alivyo simamia wanawake na Watoto sehemu mbalimbali.
Bibi Zainabu (a.s) alifariki mwezi (15 Rajabu 62h) -kwa mujibu wa kauli sahihi- na akazikwa katika viunga vya mji wa Damaskas katika Kijiji cha Rawiyah, waislamu kote duniani huenda kuzuru kaburi lake katika mji wa Damaskas, pia kuna kauli dhaifu kuwa alizikwa katika nchi ya Misri, huko pia kuna Maqaam watu huenda kuizuru na kutabaruku.