Asubuhi ya Alkhamisi mwezi (15 Rajabu-Aswabu), mawakibu za kuomboleza za mji wa Karbala zimemiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kuomboleza kifo cha mama wa misiba Aqilatu Bani Hashim bibi Zainabu (a.s).
Mawakibu zilianza matembezi katika mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi ndani ya malalo yake tukufu, kisha zikapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kuelekea katika haram ya baba wa watu huru (a.s), kuja kumpa pole bwana wa mashahidi (a.s) kwa kufiwa na dada yake bibi Zainabu (a.s) wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo hicho, kinacho huishwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia.