Kituo cha Turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina ya kuhakiki nakala-kale iliyopewa jina tukufu la mwanachuoni Mazandarani.
Kiongozi wa semina na mkufunzi Shekhe Muhammad Abdumuslim Dhwalimi amesema: “Semina hii ni sehemu ya maelekezo ya Ataba tukufu, na mazingatio ya kitengo kinacho husika na turathi za wanachuoni wetu watukufu, aidha ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu lake la kutoa mafunzo na kuandaa kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti za nakala-kale na kuziibua”.
Akaongeza kuwa: “Tumeandaa ratiba kamili ya semina, kutakua na masomo ya saa mbili kwa siku katika muda wa siku kumi, washiriki watafundishwa mambo yaote ya lazima kwa mhakiki, sambamba na kupewa majaribio, na watafundishwa kwa nadhariyya na vitendo”.
Tambua kuwa kituo cha turathi za Karbala hufanya semina mbalimbali za kuhakiki nakala-kale kielimu, bado kuna semina zingine zitakazo fanywa chini ya mkakati wa kujenga uwezo.