Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza mradi wa (Muinu-Thaqalaini) wa kuendeleza wanadamu.
Mradi huo unahusisha utoaji wa mihadhara inayo husu maendeleo endelevu ya binaadamu kutoka katika muongozo wa Qur’ani tukufu, chini ya mkufunzi wa kimataifa Ustadh Hasanaini Abaka.
Mradi unalenga wanafunzi wa Maahadi na vyuo vikuu, na taasisi za kimataifa hususan za afya na usalama, unaendeshwa katika shule za Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Baabil.
Mradi umeanza kwa kufanya semina itakayo dumu kwa muda wa siku (10) mfululizo, kila siku watasoma kwa muda wa saa (6), wahitimu watapewa vyeti vinavyo tambuliwa na umoja wa wakufunzi wa kiarabu.
Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, linafanya harakati mbalimbali za Qur’ani tukufu, pamoja na semina endelevu hapa mkoani.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’ani tukufu.