Waziri wa maji atembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Leo siku ya Alkhamisi tarehe (17 Februari 2022m) Waziri wa maji Mhandisi Mahadi Rashidi Hamdani ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mheshimiwa Waziri amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na amempongeza kwa kupewa madaraka hayo na kumtakia mafanikio mema,

Wameongea mambo mengi yanayo husiana na kutumikia wananchi, hususan katika sekta ya maji na umwagiliaji, aidha wamejadili umuhimu wa miradi ya kimkakati inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta hiyo.

Mwisho Mheshimiwa Waziri akapongeza huduma zinazotolewa na Ataba tukufu kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: