Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha dada yake

Maoni katika picha
Kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) cha harakati za wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Karbala, kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha jabali wa Subira, mama wa misiba bibi Zainabu (a.s) na kuhudhuriwa na kundi la watumishi wa kike wa Ataba tukufu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na mhadhara uliotolewa na kiongozi wa kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya bibi Adharaau Shami, ameongea mada isemayo (bibi Zainabu -a.s- ni kinara wa Subira, stara na ushujaa) amezungumza baadhi ya sifa za bibi Zainabu (a.s), ikiwa ni pamoja na kumuachia Mwenyezi Mungu kila jambo, chini ya msimamo wa dhana njema mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ilionekana katika maneno yake pale aliposema (Sikuona ispokua zuri), kila muumini wa kiume na wakike anatakiwa apambike na sifa hii, ili aishi akiwa na utulivu wa nafsi.

Majlisi ilipambwa na kaswida na tenzi kuhusu bibi Zainabu (a.s), aidha kulikua na mhadhara kuhusu kisa cha kifo chake (a.s), na kusoma ziara yake tukufu (Ziara Mufjia) na ziara Ashuraa, sambamba na hadithi Kisaa, ikahitimishwa kwa kusoma Dua-Faraji kwa ajili ya kuomba adhihiri haraka Imamu wa zama (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: