Idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa majlisi ya kuomboleza kifo cha Aqilatu-Twalibina bibi Hauraa Zainabu (a.s), ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika sardabu ya Imamu Alkaadhim (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waombolezaji.
Majlisi hiyo ni sehemu ya ratiba ya maombolezo iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhuisha msiba huu, ratiba inavipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kutoa mihadhara ya kuomboleza na kueleza historia ya bibi Hauraa (a.s) na kutaja baadhi ya utukufu na msimamo wake, na kueleza namna alivyokua akifanya ibada na kujistiri sambamba na kuhimiza wanawake wafuate mwenendo wake mtukufu.
Hali kadhalika tumefanya ibada za Ummu-Daudi kwa pamoja na kusoma dua ya Faraj, kuhuisha utiifu kwa Imamu wa zama (a.s), kisha ikasomwa ziara ya bibi Zainabu (a.s).
Majlisi imehudhuriwa na watu wengi wenye umri tofauti, na wameshiriki kikamilifu vipengele vyote vya ratiba, wameshukuru kwa kupewa nafasi ya kushiriki katika majlisi hii tukufu na kukumbuka kifo cha bibi Zainabu (a.s).
Kumbuka kuwa idara ya Qur’ani hufanya harakati za aina mbalimbali sambamba na kuonyesha dhulma walizo fanyiwa Ahlulbait (a.s) kwa njia zinazo eleweka kwa urahisi na zinazo endana na uhalisia.