Kuratibu warsha ya kielimu kuhusu njia za ufundishaji wa kisasa katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya warsha kuhusu njia za ufundishaji wa kisasa, na namna ya kunufaika nayo katika ufundishaji, mtoa mada alikua ni Dokta Ayaad Swaahibu Hamadi.

Makamo rais wa chuo Ustadh Nawaal Aaid Almayali amesema: “Warsha hii ni sehemu ya harakati za idara ya ukufunzi endelevu katika chuo, inayosaidia kufikia malengo ya kielimu kwa kuwawezesha washiriki kutumia mbinu za ufundishaji za kisasa, sambamba na mazingira ya malezi na elimu vyuoni”.

Akafafanua kuwa: “Chuo kinawapa uangalizi maalumu walimu, na huwaandalia ratiba za kuongeza vipaji na elimu zao, ili kuwafanya waendane na maendeleo ya kielimu duniani”.

Akaongeza kuwa: “Warsha imedumu kwa muda wa siku tatu, wamefundishwa njia za ufundishaji na changamato za ufundishaji sambamba na mbinu za kusimamia darasa wakati wa kuwasilisha somo, na matumizi ya vifaa vya kisasa pamoja na umuhimu wa teknolojia”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinaendelea kutoa warsha kwa watumishi wake, walimu na watumishi wengine, kwa lengo la kukuza vipaji na elimu zao, ili kuwajengea uwezo na kuwafanya waendane na maendeleo ya kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: