Kuanza mradhi wa kuwajengea uwezo mahafidh wa Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeanza kuwajengea uwezo mahafidh wa Qur’ani tukufu.

Zaidi ya mahafidh (35) wanashiriki kwenye ratiba hiyo. Mradi unalenga kuboresha kiwango cha uhifadhi na usomaji kupitia ratiba ya usomaji na mapumziko, sambamba na kutengeneza kizazi cha wasomi wanao watambua Ahlulbait (a.s).

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati mbalimbali za Qur’ani sambamba na utoaji wa semina endelevu za Qur’ani katika mkoa huo.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zofauti za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: