Waziri wa viwanda amesema: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inasaidia mambo mengi katika serikali

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo Jumamosi Mheshimiwa Waziri wa viwanda Manhal Azizi Alkhabbaaz na wajumbe aliofuatana nao, ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia huduma mbalimbali zinazotolewa katika miradi ya Ataba.

Baada ya kumaliza ibada ya ziara Mheshimiwa Waziri amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na makamo wake pamoja na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi.

Mheshimiwa Waziri amesikiliza maelezo ya baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, kama vime; miradi ya viwanda, kilimo, elimu na mingineyo, na teknolojia inayo tumika pamoja na matokeo ya miradi hiyo.

Mwishoni mwa ziara yao Mheshimiwa Waziri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumefanikiwa kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na tumekutana na viongozi wake ambao wameonyesha miradi na shughuli zinazo fanywa na Ataba takatifu, tumeona maendeleo makubwa tofauti na ziara yetu ya zamani, tumeshuhudia maendeleo mapya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tunawapongeza sana wahudumu wa Ataba”.

Akaongeza kuwa: “Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inamsaada mkubwa kwenye sekta tofauti za serikali”, akasema: “Atabatu Abbasiyya inatumia teknolojia ya kisasa katika shughuli zake, sambamba na kutumia wataalamu wa kiiraq, hii ndio furaha yetu kuona nguvukazi ya ndani inayotumika kujenga taifa letu, jambo hilo tumelishuhudia katika miradi yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Katika ziara hiyo pia wametembelea sehemu za haram ya Ataba takatifu wakiwa na rais wa kitengo cha mahusiano katika Ataba Ustadh Huquqi Muhammad Ali Azhar, wameangalia mradi wa ujenzi wa haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: