Wageni kutoka mkoa wa Dhiqaar wamesema: Tulicho kuta katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinatia matumaini ya taifa hili

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimepokea wageni ambao ni kamati ya vijana kutoka mkoa wa Dhiqaar, asilimia kubwa ni wanafunzi wa sekondari na vyuo, chini ya ratiba ya kupokea wageni kutoka mikoani.

Afisa mahusiano wa wageni hao kutoka idara ya mahusiano ya shule na vyuo Ustadh Haidari Ma’maar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Upokeaji wa wageni hawa ni sehemu ya ratiba ya kupokea wageni inayo simamiwa na kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya utendaji wa kitengo cha mahusiano ya vyuo na shule, ugeni huu umejumuisha watu wa aina tofauti, baada ya kuwapokea na kuwakaribisha wamepewa maelezo kuhusu ratiba hii na matarajio ya Ataba tukufu katika swala hili”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo ratiba ikaanza kutekelezwa kipengele kimoja baada ya kingine, miongoni mwa ratiba ilikuwa ni kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na utoaji wa mihadhara, bila kusahau mhadhara uliotolewa na Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi kutoka kitengo cha Dini, ulikua na anuani isemayo: (Njia za kufaulu katika Maisha), na warsha ya majadiliano ya wazi chini ya usimamizi wa Dokta Jasaam Saidi kutoka kitengo cha Habari, amezungumza hatua za ujenzi na ubunifu zilizofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhudumia jamii”.

Akaendelea kusema: “Hali kadhalika wamefanya ziara ya pamoja katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kutembelea korido zake tukufu”.

Mwisho wa ziara hiyo msemaji wa wageni hao bwana Saamir Jaabir, ameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema: “Pamoja na kutofautiana aina ya wageni tuliokuja lakini wote tumenufaika sawa, tumepewa maelezo mazuri yenye faida kubwa, tumekuta miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu inamustakbali mwema wa taifa letu la Iraq, miradi yote inafaida kubwa na inajibu matarajio ya kutekelezwa kwake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: