Miradi inastahiki pongezi na kujivunia.. walimu kutoka chuo kikuu cha Alkafeel wametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Walimu wa chuo kikuu cha Alkafeel wakiongozwa na wajumbe wa kamati kuu, asubuhi ya Jumapili mwezi (18 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (20 Februari 2022m), wametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia teknolojia na maendeleo ya miradi hiyo.

Rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumetembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya katika mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kuangalia mafanikio yaliyopatikana chini ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeangalia utendaji wa miradi hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Tumeona mafanikio makubwa kwenye miradi yote tuliyo tembelea, kama vile shule za Al-Ameed, na mfumo bora wa malezi unao tengeneza kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kutatua changamoto za jamii”.

Akaendelea kusema “Tumeona mafanikio makubwa kwenye miradi yote, aidha miradi yote inatumia nguvu-kazi ya wairaq na kutoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana wa kiiraq, jambo ambalo linaendana na kauli mbiu ya Atabatu Abbasiyya katika sekta zote”.

Naye mkufunzi bwana Ammaar Saadi mmoja wa wageni hao amesema: “Mwaka 2020 tulitembelea miradi ya Ataba tukufu, na leo pia tumetembelea, hakika tumekuta maendeleo makubwa tofauti na zamani, jambo hili linastahiki pongezi na kujivunia kwa namna miradi inavyo hudumia jamii na kuongeza uzalishaji wa taifa”.

Ugeni huo umetembelea (Shule ya Al-Ameed ya wasichana – maegesho ya Alkafeel – shirika la Khairul-Juud – Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji – maktaba na Daru-Makhtutwaat – kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu – kitengo cha magodauni), wamesikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa miradi hiyo.

Wakahitimisha matembezi yao kwa kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kukutana na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, amepokea wageni na akawatakia mafanikio mema ya ziara yao, na katika kutumikia sekta ya elimu na utafiti hapa Iraq, kwa namna ambayo inaendana na chuo kikuu cha Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: