Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefanya nadwa ya Qur’ani chini ya anuani isemayo (Mawaidha ya Qur’ani katika Nahaju-Balagha).
Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ukafuata mhadhara wa Shekhe Hani Rabii uliobainisha mawaidha ya Qur’ani tukufu katika Nahaju-Balagha ya kiongozi wa waumini (a.s), akaeleza maudhui za Nahaju za aina nne, miongoni mwake khutuba, barua, hekima, akasema kuwa mambo yote aliyosema kiongozi wa waumini yanatoka ndani ya Qur’ani tukufu, kwa sababu yeye ni ulimi utamkao, sambamba na kuwa alikua anabainisha Qur’ani kwa watu.
Rabii amebainisha mafundisho ya kimaadili na kimalezi yanayopatikana kwenye Nahju-Balagha baada ya Qur’ani tukufu, akawaomba vijana washikamane nayo baada ya Qur’ani, kwani kitabu hicho ndio msingi wa maelekezo na mawaidha, kinaongoza jamii katika wema.
Wahudhuriaji wamesifu mada zilizo wasilishwa kwenye nadwa, na harakati zinazofanywa na tawi hilo katika jamii.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake yote, ni tawi muhimu katika Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, linajukumu la kufundisha Qur’ani na kutengeneza jamii ya wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti za kisomi kwenye sekta zote za Qur’ani tukufu.