Kukamilika kwa shindano la kuhifadhi na kusoma Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha shindano la kuhifadhi na kusoma Qur’ani chini ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya sita, jumla ya wanafunzi (80) wameshiriki kutoka ndani na nje ya Iraq.

Shindano hilo limefanywa ndani ya ukumbi wa ofisi ya Imamu Khui (q.s) na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na viongozi wa Dini na sekula pamoja na wanafunzi wa Dini.

Kiongozi wa Maahadi Sayyid Muhanad Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini katika awamu mpya umekua na vipengele vingi, miongoni mwake ni kufanyika kwa shindano hili ambalo limepata muitikio mkubwa”.

Akaongeza kuwa “Washiriki wamepewa maswali ya jaribio kwa muda wa siku mbili katika upande wa kuhifadhi na usomaji, wameshiriki wanafunzi kutoka ngazi tofauti za hauza chini ya usimamizi wa jopo la majaji waliobobea kwenye kila fani inayoshindaniwa, jumla ya washiriki (40) wamefanikiwa kuingia katika mzunguko wa mwisho, katika kuhifadhi na usomaji wa Qur’ani”.

Kwenye mzunguko wa mwisho wamepatikana washindi wafuatao:

  • Washinzi wa usomaji:

Mshindi wa kwanza – Shekhe Husaam Alaa Jabaar.

Mshindi wa pili – Shekhe Mustwafa Muhammad Abdu.

Mshindi wa tatu – Shekhe Ali Akbaru Muhammad.

  • Washindi wa kuhifadhi:

Mshindi wa kwanza – Shekhe Ali Ridhwa Ghulamu Daanish.

Mshindi wa pili – Sayyid Jawaadina Ali Hasuun.

Mshindi wa tatu – Shekhe Hussein Swafdar Miir Hussein.

Tambua kuwa baada ya kumaliza kusoma washiriki wa shindano la kuhimadhi Qur’ani, ilifuata hafla ya kuhitimisha shindano, ambayo ilihusisha usomaji wa Qur’ani na usomaji wa surat Fat-ha kwa ajili ya kumrehemu hafidhu mkubwa wa Qur’ani tukufu (Marjaa mkuu Sayyid Abu Qassim Khui), kisha ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi Sayyid Muhanad Almayali, mwisho kabisa vikatolewa vyeti na zawadi kwa washindi na walimu watukufu.

Kumbuka kuwa jopo la majaji liliundwa na:

  • Shekhe Mudhwar Swahaaf, jaji wa kanuni za tajwidi.
  • Shekhe Mahadi Aamir. Jaji wa ubora wa kuhifadhi.
  • Shekhe Mahadi Qalandari Albayati, jaji wa kusimama na kuanza.
  • Shekhe Qudama Khadhwari, jaji wa sauti.
  • Sayyid Muhanad Almayali, jaji wa naghma za Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: