Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inafanya ufunguzi wa semina mpya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefungua semina mpya sita zenye jumla ya washiriki (111).

Kiongozi wa semina katika Maahadi Ustadhat Maasuma Kashmiri amesema: “Tumefungua semina nne kwa njia ya mtandao za wasichana wanaoishi Najafu, zenye majina yafuatayo (semina ya Batuli -a.s-, Nurul-Qur’ani, Istabraq na Firashaat), semina hizo zinajumla ya washiriki (79), wamewekwa kwa kuangalia tabaka za umri, semina mbili za wasichana wenye umri mdogo na mbili wasichana wenye umri mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Kuna semina zingine mbili zilifunguliwa pia, moja ya wasichana wa mkoa wa Karbala iitwayo (Pambo la Dini) yenye washiriki (24) na nyingine ya wasichana walio nje ya Iraq, imepewa jina la (Alqur’anul-Karim) inawashiriki (8)”.

Tambua kuwa semina hizi zimegawanyika kati ya semina za hukumu za usomaji na kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu kitakatifu.

Kumbuka kuwa semina zeto zinatumia mfumo wa elimu masafa, kwa ajili ya kutoa nafasi kwa mshiriki ya kusoma mahala popote na wakati wowote, ili asishindwe kutekeleza majikumu yake katika familia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: