Makundi ya mazuwaru yanakwenda kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alkadhim -a.s- na mawakibu zinawahudumia

Maoni katika picha
Makundi ya mazuwaru kutoka miji ya kusini mwa Iraq yanakwenda mji mkuu wa Bagdad kwa miguu, kwenda kumzuru Imamu Alkadhim -a.s- katika kumbukumbu ya kifo chake, wakiwa wamebeba bendera ya msiba na nyoyo zao zimejaa majonzi huku wakitokwa na machozi.

Barabara zinazo unganisha mkoa wa Basra na Bagdad zimejaa makundi ya mazuwaru wanaotembea kwa miguu, wanakwenda kuomboleza msiba mkubwa katika familia ya kizazi kitakatifu, msiba wa kifo cha Imamu Alkadhim (a.s).

Mawakibu za kutoa huduma zimejaa barabara zote, zinatoa huduma za lazima kwa mazuwaru watukufu, mawakibu hizo zinafanya kila ziwezalo katika utoaji wa huduma.

Wawakilishi wa mawakibu Husseiniyya wamesema kuwa wamejiandaa kikamilifu kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi, ili kutoa huduma bora zaidi katika mazingira salama na tulivu kulingana na jografia ya kila maukibu.

Kumbuka kuwa maelfu ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wameitikia wito wa kuwanusuru Maimamu wawili waliodhulumiwa na kuuawa na madhalimu, Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s) ambaye kilele cha maombolezo ya kifo chake ni mwezi ishirini na tano Rajabu-Aswabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: