Kituo cha turathi za Karbala kimehitimisha semina ya kuhakiki nakala-kale

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha semina ya kuhakiki nakala-kale, iliyopewa jina la (Semina ya mtukufu wa wanachuoni Shekhe Mazandarani q.s).

Semina imedumu kwa muda wa siku kumu sawa na saa (20) za masomo, ilikua na washiriki (35) wanafunzi wa Dini wanaofanya uhakiki.

Semina hii ni sehemu ya harakati za uongozi wa kitengo cha kujenga uwezo wa wahakiki, na kutengeneza kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kufanya uhakiki katika turathi za kiislamu na kuzihuisha kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwa njia sahihi na mbinu za kielimu zinazo endana na aina za turathi.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa kimefanya makumi ya semina katika mambo tofauti, miongoni mwake ni: Faharasi na kupangilia taaluma, uchapishaji na uhakiki wa kilugha, kwa lengo la kujenga uwezo wa wataalamu wetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: