Huduma za ugawaji wa chakula inatolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wa Imamu Alkadhim (a.s) jirani na malalo yake takatifu

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa huduma ya chakula kwa mazuwaru wa Imamu Alkadhim (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, wameweka kambi kwenye barabara inayotumiwa na mazuwaru wengi kuelekea katika malalo takatifu.

Rais wa kitengo cha mgahawa Mhandisi Aadil Hamami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, watumishi wa kitengo chetu wanatoa huduma ya kugawa chakula kwa mazuwaru kupitia Maukibu ya Ataba, chini ya ratiba maalum inayo endana na idadi ya mazuwaru hadi siku ya kilele cha ziara”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu yetu ya kutoa huduma za chakula ipo katika barabara ya Imamu Swahibu Zamaan (a.s), imepewa jina la Maukibu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inaandaa na kupika chakula halafu inakigawa kwa mazuwaru, kwa kushirikiana na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaoshiriki kwenye maukibu hio”.

Akabainisha kuwa: “Maukibu yetu inamtambo wa kuoka mikate unaohamishika, kwa ajili ya kuoka mikate na kuigawa kwa mazuwaru pamoja na vyakula vingine, wanagawa chakula kilicho wekwa kwenye vifungashio kikiwa na nyamba choma na vinginevyo, sambamba na kugawa maji, chai, matunda muda wote, wameanza kutoa huduma hizi kwa zaidi ya siku mbili zilizo pita, na tutaendelea kwa zaidi ya siku mbili zijazo”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inauzowefu mkubwa wa kuhudumia mazuwaru, inashiriki kutoa huduma kwenye zaidi ya sekta moja, inashiriki kwenye sekta ya usafiri, kugawa maji ya kunywa, kugawa chakula na vinywaji, kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani pamoja na kushiriki kwenye vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: