Idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeshiriki katika kuhudumia mazuwaru wa babu yao Imamu Mussa bun Jafari (a.s) kwenye kumbukumbu ya kifo chake, Jirani na malalo yake takatifu katika mji wa Kadhimiyya.
Kiongozi wa idara hiyo, Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ushiriki wetu katika kutoa huduma ni sehemu ya shughuli zinazo fanywa na maukibu ya Atabatu Abbasiyya iliyopo kwa sasa Jirani na malalo ya Maimamu wawili Alkadhimaini (a.s), tumeweka kambi sehemu mbili, ya kwanza mbele ya mlango wa Muradi, na sehemu ya pili mbele ya mlango wa Swahibu-Zamani (a.f)”.
Akabainisha kuwa: “Huduma zinazo tolewa na Masayyid ni kugawa chakula na vinywaji kwa mazuwaru muda wote, sambamba na kupokea mazuwaru kwa maneno mazuri na kuwapa pole, huku wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi ambayo humpa utulivu wa nafsi zaairu, utawaona Masayyid wanavyo shindana katika kutoa huduma bila kudharau hata hata jambo dogo”.
Akaendelea kusema: “Miongoni mwa huduma wanazo toa ni kufanya ziara kwa niaba ya watu waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, kazi hiyo itaendelea hadi siku ya kilele za ziara”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inauzowefu mkubwa katika kuhudumia mazuwaru, na imeshiriki katika sekta tofauti, kama vile sekta ya usafiri, kugawa maji safi ya kunywa kwa mawakibu, kugawa chakula na vinywaji kwa mazuwaru, kufungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu, sambamba na kushiriki kwenye vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.