Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika kubeba mazuwaru wa Imamu Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kubeba mazuwaru wa Imamu Alkadhim (a.s) kwa magari kadhaa yaliyo andaliwa kwa ajili ya jukumu hilo, kwenye barabara inayo tumiwa na mazuwaru wengi kwa kushirikiana na Atabatu Kaadhimiyya.

Msimamizi wa idara ya usafirishaji Ustadh Hussein Jaabir kutoka kitengo cha mitambo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huduma ya usafiri ni miongoni mwa huduma zinazotolewa na Maukibu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka katika kukumbuka kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s), kwa kutumia gari maalum za kubeba mazuwaru na kuwafikisha karibu na malalo takatifu”.

Akaongeza: “Gari zinazotoa huduma zipo (30) za ukubwa tofauti, tumeanza kutoa huduma sambamba na vikosi vya ulinzi na usalama, baada ya kuainisha barabara zitakazo tumika kubeba mazuwaru watukufu”.

Akabainisha kuwa: “Ushiriki haukuishia kwenye usafirishaji pekeyake, bali kunasekta mbalimbali ambazo gari za Ataba tukufu zinatoa huduma, ikiwa ni pamoja na gari maalum za kusambaza maji kwa mawakibu, kuna gazi za usafi, gari za kusambaza gesi za kupikia, kazi zote zimewekwa katika zamu mbili ya Asubuhi na jioni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: