Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kufanya ziara ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake na mbele ya kaburi lake katika mji wa Kadhimia kwa niaba.
Kila mtu anayependa kufanyiwa ziara kwa niaba ajisajili kwenye ukurasa wetu wa ziara kwa niaba kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/
Atafanyiwa ziara na mmoja wa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) miongoni mwa masayyid, watafanya ziara ya Imamu Alkadhim na mjukuu wake Jawaad (a.s) na swala ya rakaa mbili kwa niya ya kukidhiwa haja na kurahisishiwa mambo, kwa niaba ya kila atakaejisajili na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao.