Watumishi wa malalo mbili takatifu wanaomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wanaomboleza kupitia maukibu ya pamoja, wanahuisha utiifu kwa kinara wa elimu na hekima mlango wa haja Mussa bun Jafari (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, aliyefariki siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Rajabu.

Maukibu ya kuomboleza imeanza matembezi baada ya Adhuhuri ya leo siku ya Jumapili mwezi (25 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (27 Februari 2022m), chini ya utaratibu wa mikusanyiko na harakati maalum katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamesimama kwa mistari na kwenda kutoa pole ya msiba huo.

Baada ya hapo Maukibu ikaenda kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, ikiwa imetanguliwa na jeneza la kuigiza pamoja na bendera zinazo ashiria msiba, wakiwa wamejaa huzuni kutokana na kifo cha Imamu wao aliyeuawa kwa sumu.

Maukibu ilipo wasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) ikapokewa na watumishi wa haram hiyo na wakaungana na kuomboleza kwa pamoja, wakafanya ibada ya ziara kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza na kusoma tenzi zilizo amsha hisia ya huzuni kutokana na msiba huo, ulio umiza moyo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), uliotokea katika siku kama ya leo mwaka wa 183h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: