Waziri wa ulinzi Mheshimiwa Juma Inaad Saaduni asubuhi ya leo Jumatatu tarehe (28 Februari 2022m) ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Amepokewa na makamo rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Jalukhaan.
Katika ziara hiyo; Waziri amefuatana na kamanda wa vikosi vya Karbala na kamanda wa polisi wa mkoa pamoja na viongozi wengine wa usalama kutoka wizarani.