Chapisho la kituo cha turathi za Hilla limefuzu kwenye shindano la kitabu bora cha hauza katika mji wa Qum

Maoni katika picha
Vitabu vitatu vya kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislsmu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vimeshinda kwenye shindalo la vitabu vya hauza ambalo hufanywa kila mwaka nchini Iran/ katika mji mtukufu wa Qum, mwaka huu ni awamu ya ishirini na mbili ya shindano hilo.

Machapisho yaliyoshinda ni:

  • 1- Mafaqihi wa Fihaa na kuendelea kwa harakati za kifikra katika mji wa Hilla.
  • 2- Kufichua yaliyofichikana katika sifa za Mahadi (a.f).
  • 3- Majibu ya mambo ya kazi.

Hii ni mara ya tatu kituo cha turathi kinapata ushindi kwenye shindano hilo, mara ya kwanza kilishinda kwenye mashindano mawili na kupata zawadi mbili ya kitabu cha (Mausua Rijaliyya cha Allaamah Alhilliy) na kitabu (Mukhtasar Maraasim Alawiyya).

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hillah kinafanya kazi ya kuhakiki na kuandika vitavu, kinaidara mbalimbali na watumishi wenye uzowefu mkubwa katika fani zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: