Siku ya mwezi ishirini na saba katika mwezi wa Rajabu ni kumbukumbu ya kupewa Utume na kushuka Jibrilu (a.s) na ujumbe wa Utume, nayo ni siku tukufu sana, ndio siku ya kwanza ya Utume wa Muhammad (s.a.w.w).
Kupewa Utume ni kushuka kwa nuru na kuletwa Qur’ani tukufu na kuanza mafundisho ya kiislamu, hakika siku hiyo ni siku kuu, sio kwa waislamu peke yake bali kwa wanaadamu wote, Utume wa Muhammad (s.a.w.w) na baraka zake zimeenea kwa viumbe wote.
Riwaya zinaonyesha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipewa Utume siku ya Jumatatu mwezi ishirini na saba Rajabu, miaka kumi na tatu kabla ya kuhama (Hijra), na miaka arubaini baada ya mwaka wa tembo na miaka (610) baada ya kuzaliwa (miladi).
Kupewa Utume kuliambatana na kushuka kwa wahyi, naye ni Malaika mtukufu Jibrilu (a.s) aliyekuja kumuambia kuwa Mwenyezi Mungu amemteua kuwa Mtume, wahyi huo ulienda sambamba na kushuka aya za Qur’ani tukufu.
Imamu Ali bun Abu Twalib kiongozi wa waumini (a.s) anasema, kuhusu kupewa Utume kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa: (Alipewa Utume watu wakiwa katika upotevu, wamezama katika fitna, wanatii matamanio yao, wamepotoshwa na kiburi, ujinga umeenea, wamechanganikiwa na tatizo la ujinga, akaanza kuwanasihi, akaendelea na kazi hiyo kwa hekima na naneno mazuri).
Bibi mtukufu Fatuma Zaharaa (a.s) anasema katika hutuba yake kuwa: “Mlikua pembezoni mwa shimo la moto, uunguzao masharubu, unaotamanisha wenye tamaa, uwakao haraka, uunguzao miguu, mnakunywa risasi na kutema karatasi, madhalili wenye hasara, {mnaogopa kuzingirwa na watu}, Mwenyezi Mungu mtukufu akakuokoweni kwa kumlewa Muhammad (s.a.w.w)”.
Akasema pia: “Umma ukaona kundi katika dini yake, wamesimama juu ya moto, wanaabudu masanamu, wanamkanusha Mwenyezi Mungu pamoja na kumfahamu kwao, Mwenyezi Mungu akang’arisha dunia kwa nuru ya Muhammad, akaondoa giza katika nyoyo na mawingu katika macho, akasimama mbele ya watu na kufundisha uongofu, akawaokoa katika maangamizi, akawaonyesha njia sahihi na kuwaongoza katika Dini na kuwaelekeza katika njia iliyo nyooka”.
Amma aya alizoshusha Jibrilu (a.s) kwa Mtume (s.w.w.w) ni aya tano za mwanzoni mwa surat Alaq, ambazo ni: (Kwa jina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba * Amemuumba mwanaadamu kwa pande la damu * Soma na Mola wako ni mtukufu * Ambaye amefundisha kwa kalamu * Amemfundisha mwanaadamu asiyofahamu).
Mtu wa kwanza aliyemlingania; alikua ni mke wake Khadija (a.s) na mtoto wa Ammi yake Ali bun Abu Twalib (a.s) akiwa na umri wa miaka kumi, wakamuamini na kumsadikisha, wakawa mbegu ya kwanza katika uislamu mtukufu.