Hivi karibuni idara ya Habari chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa muongozo mpya kwa jina la (Muongozo wa shindano la maarifa ya turathi kwa vikundi katika mwezi wa Ramadhani).
Muongozo huo unamaelekezo ya shindano, kuanzia idadi ya washiriki kwenye kila kikundi, aina ya shindano, malengo ya shindano na ufanyaji wa shindano na matokeo yake.
Muongozo huo unaidadi kubwa ya picha zinato onyesha matukio ya shindano hilo kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho.
Muongozo huo ni sehemu ya machapisho yanayofanywa na kitengo cha maarifa yakutunza taarifa ya harakati zote wanazofanya, na mafanikio yaliyopatikana, kwa ajili ya kuyarusha kwenye vyombo vya Habari, na kuyahifadhi yasipotee na kusahaulika, na kuanzisha albamu kamili kwa kila kazi.
Kumbuka kuwa idara ya Habari na maarifa imechukua jukumu la kuandaa muongozo huo, na imekamilisha kwa kiwango kikubwa, kuna miongozo mingine itakamilika hivi karibuni.